Monday, February 27, 2012

Magufuli amkaba koo mkandarsi Arusha  
Monday, 27 February 2012 18:38

Waziri wa Ujenzi,Dk John Magufuli
Filbert Rweyemamu, Arusha
WAZIRI  wa Ujenzi, Dk John Magufuli ameipa siku saba kampuni ya ujenzi ya  Satos kutoka nchini Ufaransa, iwe imeanza kazi za awali za ujenzi wa barabara ya Arusha hadi Minjingu vinginevyo itakuwa imekosa sifa na atalazimika kuwakuza mara moja.

Mbali ya kutoa siku saba kwa mkandarasi huyo, Dk Magufuli pia amekataa mpango wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) mkoa wa Arusha, kutaka kuuza mitambo miwili ya kutengeneza barabara badala yake inapaswa karabatiwe ili itumike kwa ujenzi wa barabara na kukodishwa  kwa wakandarasi.Dk Magufuli alitoa kauli hiyo juzi wakati akiweka jiwe la msingi la msingi katika majengo mawili ya makazi na biashara yenye ghorofa kumi kila moja katika mtaa wa  Wachaga na Wasukuma na jengo la makazi katika mtaa wa Simeon mjini Arusha kuwa  serikali haitavumilia kuona fedha ilizokopa zinachezewa.

“Nashangaa kuona hata hawajafanya mobilazition kwenye eneo waliloomba kazi,ninawapa siku saba,meneja wa Tanroad uwaambie wakishindwa kufanya kazi iliyowaleta nawatimua,tumekopa kiasi cha Sh.78 bilioni za watanzania wote kama hawezi nitamtimua hapa nchini,”alisema Magufuli

Alisema kwa sasa hapa nchini kuna Makandarasi wazawa wapatao 9000 katika madaraja tofauti hivyo hakuna haja ya kuendelea kuwabembeleza makandarasi wa kigeni wanachezea fedha za watanzania bila kutekeleza wajibu wao.

Magufuli aligeuka mbogo kwa TEMESA baada ya kuwaagiza kuacha mara moja mpango aliusikia wa kuuza mitambo miwili ya kujenga barabara na kuwa taka kuitengeneza ikodishwe katika shughuli za ujenzi.“Kwanini mnataka kuiuza?nyie si mnaitwa  mainjinia,nataka muitengeneze mara moja kama kuna vipuri mvitafute ili hiyo mitambi iweze kufanya kazi,”alisisitiza Magufuli

Kabla ya kuweka jiwe la msingi, alisema nchi nzima inakabiliwa na uhaba wa nyumba zipatazo milioni tatu na Wizara yake kupitia Wakala wa Majengo itaendelea kujenga nyumba kila mwaka na kuwa mwaka huu wa fedha imeshajenga zaidi ya nyumba 1043 katika mikoa mbalimbali.


Alisema kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la makazi duniani,inaonesha  wananchi kati ya asilimia 70 hadi 75 wanaishi katika makazi duni hivyo serikali itahakikisha inaboresha makazi  kulingana na uwezo wake.


Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Dk John Ndunguru, aliwataka TBA kuhakikisha ujenzi wa mradi huo unakwenda kwa kasi na muda kama ilivyopangwa, huku akisisitiza weledi na uadilifu katika utekelezaji.

Mhandisi Dk Ndunguru alisema mradi huo ni muhimu kwa taifa hivyo, ni vema ukafanyika kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha lengo la kubuniwa kwake linakamilika.


Awali, KaimuMtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini(TBA), Elius Mwakalinga alisema wakala huo unahitaji kiasi cha Sh.5 bilioni ili kukamilisha ujenzi wa majengo hayo mawili yatakayopunguza uhaba wa nyumba mkoani Arusha kutokana na umuhimu katika utalii na mashirika ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment