Siyoi Sumari aitesa CCM
HATIMAYE yametimia. Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimetangaza kwamba, kura za maoni katika Jimbo la Arumeru Mashariki ndani ya chama hicho, zitarudiwa.
Uamuzi huo, ulitangazwa mjini Dar es Salaam jana na Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema watakaoshiriki katika mpambano huo, ni aliyekuwa mshindi wa kura za awali, Siyoi Sumari na mshindi wa pili, William Sarakikya.
Katika mazungumzo yake, Nape alisema kura hizo zitarudiwa kesho kutwa, kwa kuwa Siyoi hakupata nusu ya kura zilizokuwa zinahitajika.
Katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita, Siyoi aliibuka mshindi kwa kupata kura, 361, Sarakikya alipata kura 259 na aliyeshika nafasi ya tatu alikuwa ni Elirehema Kaaya aliyepata kura 176.
Mshindi wa nne, alikuwa ni Antony Msami aliyepata kura 22 na aliyefuata alikuwa ni Moses Urio aliyepata kura 11.
Pamoja na CCM kutangaza uamuzi huo, jana MTANZANIA iliripoti kwamba, CCM iko katika mkakati mzito wa kumng’oa Siyoi jimboni humo, ili nafasi yake ichukuliwe na Sarakikya.
Taarifa za uhakika zilizokuwa zimepatikana kutoka vyanzo vyetu vya habari, zilisema CCM wanataka kufanya uamuzi huo kwa kigezo kwamba, Siyoi ambaye ni mtoto wa marehemu Jeremia Sumari, si Mtanzania, bali ni Mkenya kwa kuwa alizaliwa Kenya.
Chini ya mkakati huo, unaoungwa mkono kwa nguvu zote na baadhi ya viongozi wa chama hicho, CCM wanataka kumsimamisha William Sarakikya kwa kuwa wanaamini anakubalika na ana uwezo wa kuhimili vishindo vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Habari hiyo ilieleza kuwa, viongozi wanaosimamia mkakati wa kumng’oa Siyoi unaongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira.
Vile vile juzi MTANZANIA, ilisema Sekretarieti ya CCM ilikutana Jijini Dar es Salaam na kukubaliana kuwa, baada ya Siyoi kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho, walioshiriki kura za maoni za CCM na kushindwa, watakutanishwa na kushawishiwa ili wamuunge mkono Sarakikya na pia warudishiwe gharama walizotumia kwenye kampeni.
Pia wajumbe wa kikao hicho walikubaliana kumwagiza Siyoi alete nyaraka zake kuonyesha uraia wake kabla ya Kikao cha Kamati Kuu kilichokaa jana na kupitisha mabadiliko hayo.
Hoja nyingine, iliyojengwa na wana CCM hao katika kikao hicho, ni kwamba Siyoi hakushinda kwa zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa.
Akizungumza kwenye mkutano wake na waandishi wa habari jana, Nape alitetea uamuzi huo na kusema umepitishwa na Kamati Kuu iliyokutana jana mjini Dar es Salaam.
“Zoezi la kura za maoni litarudiwa Machi mosi, Machi 2 Kamati ya Siasa ya Mkoa, itakutana na kupitia kura kabla ya kutangaza jina la mshindi, Machi 3.
“Watakaosimamia mchakato huu, ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Mzee wetu Pius Msekwa, Naibu Katibu Mkuu, Tanzania Bara, Kapteni John Chiligati na Mjumbe wa Baraza la Vijana la Taifa la UVCCM, Constansie Buhie,” alisema Nape.
Kuhusu suala la uraia wa Siyoi, Nape alisema suala hilo halina ushahidi na kwamba hata wao walipohitaji ushahidi wa kina kuhusu jambo hilo, haukupatikana ushahidi wa kutosha.
“Hizi tuhuma kuwa Sumari ameponzwa na makundi ya ndani ya CCM, hazipo na wanaoshangazwa na utaratibu wa kurudiwa kura wajue siyo mpya, bali ni wa kawaida ndani ya CCM,” alisema.
Baada ya mabadiliko hayo kutangazwa, taarifa zilizolifikia MTANZANIA zinasema, kuna mkakati mzito uliopangwa na vigogo ndani ya CCM waliokuwa wakimpinga Siyoi, kwamba wanajipanga kuhakikisha Sarakikya anashinda katika mchujo huo wa pili.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, vigogo hao jana waliwasili Jijini Arusha kwa moja ya ndege za Shirika la Ndege la Precision.
Taarifa hizo, zinaendelea kusema vigogo hao, wanafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha Sarakikya anashinda na kwamba hivi sasa zinafanyika jitihada za kuwashawishi walioshindwa katika kura za maoni wamuunge mkono Sarakikya wakati wa kampeni.

No comments:
Post a Comment