Watu wenye silaha nchini Somalia walimpiga risasi na kumuuwa mkurugenzi wa kituo cha radio ambacho kilifungwa na kundi la wanamgambo la alshabab mwaka 2010. Mashahidi waliiambia Sauti ya Amerika  kwamba Abubakar Hassan Kadaf alishambuliwa na watu wawili wakiwa na bastola Jumanne usiku alipokuwa akirudi nyumbani kwake Mogadishu. Alithibitishwa kuaga dunia kwenye hospitali ya mji huo. Haikubainika mara moja ni nani aliyemwua. Muungano wa waislam  Somalia ulilaani mara moja mauaji hayo na kusema kwamba Kadaf alikuwa ni mkurugenzi wa pili kuuawa Mogadishu katika kipindi cha mwezi  mmoja uliopita. January 28 watu wenye silaha walimuuwa Hassan Osman Abdi mkurugenzi wa Radio Shabelle.